[SWAHILI] Islam – Hadith : Fadhla za Swala ya Sunna.

Swala ya Sunna : Swala iliyowekwa na Sheria isiyokuwa ya lazima.

IMG_20161101_094943

Fadhla za Swala ya Sunna

1. Swala ya sunna ni sababu ya mja kupendwa na Mwenyezi Mungu. Imekuja kwenye hadithi Alqudusiy kwamba Mwenyezi Mungu Aliyetukuka ansema: (Haachi mja wangu kuendelea kujikurubisha kwangu kwa sunna mpaka nimpende, na ninapompenda nitakuwa ni masikizi yake ya kusikia na maangalizi yake ya kuonea na mkono wake wa kushikia na mguu wake wa kuendea, na akiniomba nitampa, na akijilinda kwangu nitamlinda) [Imepokewa na Bukhari.]

2. Swala ya sunna inaunga kasoro za faradhi. Mtume ﷺ amesema: (Kitu cha kwanza wanachohesabiwa kwacho Siku ya Kiyama miongoni mwa matendo ni Swala. Mwenyezi Mungu aliyetukuka, Atawaambia Malaika wake- na yeye ni mjuzi zaidi-: “Itizameni Swala ya mja wangu, je ameikamilisha au ameipunguza?” Iwapo imekamilika inaandikwa kuwa imekamilika, na ikiwa ina upungufu wa kitu, Atasema: “Tizameni, je mja wangu huyu ana sunna alizoziswali? Akiwa ana sunna, Atasema: Mkamilishieni mja wangu faradhi yake kutoka kwa sunna zake” ) [Imepokewa na Abu Daud.].

3. Swala ya sunna nyumbani ni bora zaidi

Swala ya sunna majumbani ni bora kushinda misikitini isipokuwa katika Swala ziliwekewa jamaa na Sheria kama Swala ya Tarawehe katika mwezi wa Ramadhani. Mtume ﷺ amesema: (Bora zaidi wa Swala ya mtu ni ile anayoiswali nyumbani kwake isipokuwa Swala ya faradhi) [Imepokewa na Bukhari.]

 


Aina za Swala ya sunna

Swala ya sunna ni aina nyingi: Muhimu zaidi ya hizo ni zifuatazo:

Kwanza: Sunna za ratiba

Nazo ni sunna zenye kufuata Swala za faradhi

Na jumla ya sunna za ratiba ni rakaa kumi au rakaa kumi na mbili, nazo ni:

– Rakaa mbili kabla ya Alfajiri.

– Rakaa mbili kabla ya Adhuhuri au nne na rakaa mbili baada yake.

. Rakaa mbili baada ya Magharibi.

– Rakaa mbili baada ya Isha. Ibnu ‹Umar amepokewa akisema: (Nimehifadhi kutoka kwa Mtume ﷺ rakaa kumi: Rakaa mbili kabla ya Adhuhuri na rakaa mbili baada yake, rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, rakaa mbili baada ya Isha nyumbani kwake na rakaa mbili kabla ya Swala ya Asubuhi) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Na imethubutu hadithi kama hii kutoka kwa ‘Aishah t isipokuwa yeye alitaja rakaa nne kabla ya Adhuhuri [Imepokewa na Muslim.]


Na bora wa sunna za ratiba ni ambazo Mtume ﷺ alidumu nazo mjini na safarini ni rakaa mbili za Alfajiri, kwa hadithi ya ‹Aishah t kwamba alisema: (Mtume ﷺ hakuwa akidumu na kitu chochote miongoni mwa sunna isipokuwa rakaa mbili za Alfajiri) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Na imesunniwa kuzifanya fupi rakaa zake bila kuziharibu wajibu wake, kwa ilivyothubutu kutoka kwa Aishah t kuwa alisema: (Alikuwa Mtume ﷺ akizifupisha zile rakaa mbili za kabla ya Swala ya Asubuhi kwa kiasi kwamba nilikuwa nikisema: “Je amesoma Fatiha?”) [Imepokewa na Bukhari.]

.

source : sw.islamkingdom.com


 

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *